Rafiki yangu, karibu..
I'm so happy that you are here..
Naitwa Cesilia Mgimwa. Na hizi ni fact chache kuhusu mimi;
1. Mimi ni Childhood Trauma Survivor
2. Nimeanza kujifunza kusoma na kujifunza Saikolojia ya tabia na ukuaji miaka 10 iliyopita.
3. Mentors wangu wakubwa ni Dr. Gabor Mate (Kwenye eneo la Childhood Trauma), Dr. Daniel Goleman ( Kwenye eneo la Emotional Intelligence), Dr. Snipe (Mkufunzi wangu wa Trauma-Informed Certificate), Dr. Shefali Tsabary (Kwenye eneo la conscious Parenting).
4. Mimi ni Certified Trauma Informed Coach.
5. Nilipanua uelewa wangu wa Saikolojia nilipopata nafasi ya kuishi Korea kusini.
6. Pamoja na kuwa Trauma Informed coach, mimi ni Entrepreneur (Running a skincare consultancy & Distribution Company in Tanzania), Certified Skincare Consultant na Business Strategist (MBA)
7. Kwenye website yangu, natumia vyote Kiingereza na Kiswahili
8. Kwa Takribani miaka 10 nimekuwa nikisoma au kusikiliza chochote kuhusu Saikolojia karibu kila siku.


Ukweli ni kwamba..
Mapenzi yangu ya Saikolojia ya tabia yalianza tangu nikiwa na umri mdogo. Nilivyofika "teenage" nilianza kuona baadhi ya patterns za tabia kwangu ambazo hazikuwa nzuri na zilininyima furaha. Patterns hizi niliziona hasa kwenye eneo la mahusino ya kimapenzi na hata urafiki.
Kwa bahati nzuri nilijua fika kuwa patterns za tabia zile si rafiki na zenye afya kwa furaha na maisha yangu ya mbeleni lakini iliniwia vigumu mno kubadilika.Mara kwa mara nilihisi labda ninarogwa. I knew for sure something wasn't right.
Nilipopata nafasi ya kwenda South Korea na kukutana na watu kutoka nchi tofauti tofauti, niliona namna gani tabia na mtazamo wetu katika mambo mbalimbali ulivyo tofauti. I knew for sure, our personality and thinking are influenced by our background and early experiences. Hapo ndipo niliamua kujifunza kwa undani na kuanza kuexplore therapy ili kuielewa tabia yangu na hasa kwenye yale mambo yaliyokuwa yakinirudisha nyuma. Nilipoanza kujifunza na kuexplore therapy, A lot of things started to make sense in my life. Na nikawa na "ahaa" moments nyingi.
​
Kupona kutoka kwenye Childhood Trauma ni safari ndefu. Lakini at least ukijua your triggers na ukaelewa baadhi ya patterns zinazoleta changamoto kwenye maisha yako, inakusaidia sana kuwa conscious kwenye maamuzi yako na mtindo wako wa maisha.